pmbet

Makamanda wa kijeshi jijini Khartoum kuondoa vikosi vyao

Eric Buyanza

August 11, 2025
Share :

Makamanda wa kijeshi jijini Khartoum jana Jumapili wameahidi kuondoa vikosi vyao kwenye mji huo na kwamba hawatawaunga mkono wapiganaji wowote watakaosalia baada ya makubaliano ya mwisho ya kusitisha vita. 

Ahadi hiyo  ilitolewa wakati wa mkutano wa kamati ya serikali iliopewa jukumu la kumaliza vikundi vya kijeshi kwenye mji huo.
Hatua hii ni sehemu ya juhudi za kuondoa vikundi vya kijeshi na kuruhusu maelfu ya raia waliokimbia makazi yao kutokana na vita kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa RSF kurejea kwenye maisha yao ya kawaida.

Mnamo mwezi Julai 18, kiongozi wa kijeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan aliunda kamati ya kufuatilia kuondolewa kwa makundi yenye silaha na kuandaa kurejea kwa raia kwenye mji huo.

Hatua hii ya kuyaondoa makundi yaliojihami inatazamwa kuwa muhimu wakati huu serikali ikipanga kurejea mjini Khartoum kutoka katika makao yake ya sasa ya Port Sudan.

Wiki iliopita, Waziri Mkuu kamil Idris alitangaza kuwa taasisi za serikali zitarejea jijini Khartoum mwezi Oktoba mpango uliosambamba na kufunguliwa tena kwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet