pmbet

Makumbusho ya Taifa yamkumbusha Rais wa Finland Chimbuko lake.

Joyce Shedrack

May 16, 2025
Share :

Rais wa Jamhuri ya Finland Mhe. Alexander Stubb afurahishwa na uhifadhi wa historia uliohifadhiwa katika kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.

Akiongea katika ziara maalum aliyoifanya kituoni hapo Mei 15,2025, Mhe. Rais Stubb amesema “kwa sasa natambua chimbuko langu (Now, I know where I came from)”, kauli ambayo imetokana na kujionea historia adhimu ya chimbuko la mwanadamu.

 

Naye mwenyeji wake Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), Waziri wa Maliasili na Utalii amekumbushia ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Finland ni wa kihistoria kwa kutaja ushahidi wa marais waliopita kutoka Tanzania kutembelea Finland kuanzia Rais wa kwanza Mwl. JK Nyerere, Rais Benjamin Mkapa, Rais Jakaya Kikwete na hatimaye Rais Samia Suluhu Hassan.

 

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania Dkt. Noel Lwoga amewahimiza watanzania na wadau mbalimbali kutembelea maeneo ya Makumbusho na Malikale ili kufahamu historia na asili yao.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet