pmbet

Mali kumuongezea kiongozi wa kijeshi miaka 5 madarakani

Eric Buyanza

June 12, 2025
Share :

Baraza la Mawaziri nchini Mali limeidhinisha mswada tata wa sheria unaompa kiongozi wa kijeshi miaka mingine mitano ya kukaa madarakani. 

Jenerali Assimi Goita ameliongoza taifa hilo la magharibi mwa Afrika tangu alipofanya mapinduzi mwaka 2021.

Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa utawala wa kijeshi kuvipiga marufuku vyama vya siasa mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa tamko la baraza hilo, muswaada huo utafanya mapitio ya kile kiitwacho "Mkataba wa Kipindi cha Mpito" ili kumpa mkuu wa nchi muhula wa miaka mitano "unaoweza kurefushwa kuanzia mwaka huu wa 2025."

Sheria hiyo mpya inadaiwa kuakisi mapendekezo ya majadiliano ya kitaifa yaliyogomewa na vyama vya siasa mnamo mwezi Aprili.

Mswaada huo wa sheria unangojea sasa kupitishwa na Baraza la Mpito la Taifa, ambalo ni kama bunge linalosimamia kipindi cha mpito.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet