Mama Dangote asema akifa Diamond Platnumz atateseka sana.
Joyce Shedrack
October 11, 2025
Share :
Mama mzazi wa staa wa muziki wa bongofleva Nchini Diamond Platnumz Bi Sandra maarufu Mama Dangote amesema kama ikitokea akafariki basi kijana wake Diamond Platnumz atateseka sana.

Mama Dangote ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram alipochapisha picha mjongeo akiwa na mwanae akiambatanisha na ujume kuwa amerudi safari akaenda kwa mama kudeka.
“CHAKUDEKA WANGU!! TOM KAKA KARUDI SAFARI SASA ANADEKA KWA MAMA RS YANI NIKIFA ATAPATA TABU SANA HUYO MTOTO @diamondplatnumz LAKINI MTOTO KWA MAMA HAKUI”- Ujumbe kutoka kwa Mama Mzazi wa Staa huyo wa muziki.