pmbet

Mama Maria Nyerere atimiza miaka 94 ya kuzaliwa

Sisti Herman

December 31, 2024
Share :

 

Leo ni siku muhimu na maalum ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mpendwa Mama yetu wa Taifa, Mama Maria Nyerere, ambaye leo ametimiza umri wa miaka 94, akiwa ni mfano bora wa hekima, upendo, na uvumilivu, ambavyo ni alama isiyofutika katika historia ya taifa letu.

Mama Maria Nyerere (alizaliwa kama Maria Waningu Gabriel Magige mnamo 31 Disemba 1930) ni mjane wa Baba wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Raia wa nkwanza wa Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi 1985. Na anajulikana zaidi kama 'Mama Maria.'

Mama Maria alikuwa mtoto wa saba kati ya watoto tisa wa Mzee Gabriel Magige, kutoka Baraki, Tarime, na mkewe Hannah Nyashiboha.

Mama Maria alisoma katika shule ya "White Sisters' School" iliyokuwa Nyegina, kisha alijiunga na shule ya Ukerewe. Baadaye alijiunga na Chuo cha Ualimu cha Sumve, ambapo alihitimu kwa kupata cheti cha ualimu na kuanza kufundisha katika Shule ya Msingi ya Nyegina, iliyoko Musoma.

Mama Maria alifunga ndoa na Mwalimu Nyerere mwaka 1953. Katika maisha yao ya miaka 45 ya ndoa walijaaliwa watoto saba na zaidi ya wajukuu 22.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet