Mamelodi mabingwa wa Afrika Kusini kwa mara ya 8 mfululizo.
Joyce Shedrack
May 14, 2025
Share :
Klabu ya Mamelodi Sundowns wametangazwa rasmi kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini kwa msimu wa 2024/25 kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Chippa United usiku huu huku wakifikisha alama 70 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote baada ya michezo yote ligi.
Masandawana wanaonolewa na Miguel Cardoso wametwaa ubingwa huo kwa mara ya 8 mfululizo huku likiwa ni taji lao la 15 la ligi kuu Nchini humo.