Man U na Tottenham kwenye vita ya kumnunua Rayan Cherki
Eric Buyanza
April 30, 2025
Share :
Man United na Tottenham wako tayari kuchuana katika kinyang'anyiro cha kuwania saini ya nyota wa Lyon, Rayan Cherki.
Lyon huenda ikalazimika kumuuza winga huyo mwenye umri wa miaka 21 kutokana ukata wa kifedha unaoikabii klabu hiyo.
Cherki amekuwa na msimu mzuri, akifunga mabao 12 na kutoa asisti 19 katika michezo yake 41 katika mashindano yote.
Kwa mujibu wa taarifa, Lyon inataka kitita cha Euro milioni 35 ili iweze kumuachia winga huyo.