pmbet

Man U yathibitisha kuondoka Eriksen, Evans na Lindelof

Eric Buyanza

May 26, 2025
Share :

Manchester United imethibitisha kuondoka wachezaji Christian Eriksen, Jonny Evans pamoja na Victor Lindelof.

 

Wachezaji wote watatu walishiriki kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Aston Villa siku ya mwisho ya msimu, huku Eriksen akifunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti.

 

Watatu hao wamecheza zaidi ya mechi 600 wakiwa Man U na jana Jumapili walitoa mkono wa kwaheri kwa kuwapungia mkono mashabiki.

 

Taarifa ya klabu hiyo ilisomeka: "Kila mtu United anawashukuru Victor, Jonny na Christian kwa michango yao wakati walipokuwa Old Trafford, na inawatakia kila la kheri kwa siku zijazo. "Kila mmoja wao alipokea shangwe kubwa kutoka kwa umati wa watu wenye shukrani siku ya Jumapili."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet