Man United na Spurs kuumana leo fainali ya Europa League
Sisti Herman
May 21, 2025
Share :
Fainali ya UEFA Europa League leo, Mei 21, 2025, itawashirikisha Tottenham Hotspur dhidi ya Manchester United kwenye Uwanja wa San Mamés huko Bilbao, Hispania. Mechi itaanza saa 8:00 PM (saa za Uingereza) au saa 4:00 AM (saa za Afrika Mashariki, Mei 22, 2025).
Dondoo muhimu kuelekea mchezo huu.
Manchester United: Wao ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo katika mashindano makubwa ya Ulaya msimu huu, wakiwa na ushindi 9 na sare 5 katika mechi 14 za Europa League.
- Wamefunga magoli 35, idadi ya pili kwa juu katika historia ya UEFA Cup/Europa League.
- Bruno Fernandes ameongoza kwa magoli 7 na asisti 4, huku Mason Mount, Casemiro, na Rasmus Højlund wakiwa wachezaji muhimu.
- Kocha Ruben Amorim anaweza kuwa kocha wa tatu kushinda taji kubwa katika msimu wake wa kwanza na United.
- Leny Yoro, Diogo Dalot, na Joshua Zirkzee wamerudi mazoezini, lakini Lisandro Martinez na Matthijs de Ligt wako nje kwa majeraha.
Tottenham Hotspur: Wanatafuta taji lao la kwanza la kimataifa tangu UEFA Cup ya 1983-84 na taji lao la kwanza la Ligi tangu 2007-08. Wameshinda mechi 9 kati ya 14 za Europa League msimu huu, rekodi yao bora zaidi.
- Dominic Solanke amefunga mabao 5 dhidi ya United katika mechi zake nne za mwisho.
- Hata hivyo, wanakosa wachezaji muhimu kama Dejan Kulusevski (kwa jeraha la goti), James Maddison, Lucas Bergvall, na Radu Dragusin (asiyestahiki).
- Kocha Ange Postecoglou ni kocha wa kwanza wa Australia kufikisha timu kwenye fainali ya Ulaya.