Man Utd kuwakaribisha Spurs leo Old Trafford
Sisti Herman
September 29, 2024
Share :
Klabu ya Manchester United leo itashuka dimbani kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza wakiwaalika kwenye dima lao la nyumbani Old Trafford klabu ya Tottenham Hotspurs.
Hadi sasa kwenye msimamo wa ligi hiyo United wapo sawa na Spurs wote wakiwa na alama 7 baada ya michezo mitano huku Spurs akiwa juu ya United kwa tofauti ya magoli.