pmbet

Martinez amwaga machozi akiwaaga mashabiki wa Aston Villa.

Joyce Shedrack

May 17, 2025
Share :

Golikipa wa Timu ya Taifa ya Argentina na klabu ya Aston Villa Emiliano Martinez usiku wa jana alimwaga machozi akiwaaga mashabiki wa klabu yake ikiwa ni mchezo wake wa mwisho kucheza akiwa na uzi wa Villa katika uwanja wa nyumbani.

Emiliano Martinez: Unai Emery coy on Aston Villa goalkeeper's future - BBC  Sport

Martinez ambaye amekuwa na kiwango bora tangu ajiunge na Aston Villa mwaka 2020 anahusishwa kutimkia ligi kuu ya Saudia Arabia baada ya kupokea ofa nyingi licha ya kuwa bado hajafanya maamuzi ya mwisho.

 

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 alionekana akimwaga machozi huku akiwaaga mashabiki wa Villa kwenye mchezo wa jana wa ligi kuu Uingereza walipowakaribisha Tottenham na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-0.

 

Akizungumza baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Aston Villa Unai Emiry amesema “Huu ni mchezo wetu wa mwisho hapa nyumba kuhusu Emiliano Martnez sijui lakini tutaona huko mbele”.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet