pmbet

Mashabiki kupendezesha B.Mkapa na rangi nyekundu siku ya Fainali ya CAF.

Joyce Shedrack

May 12, 2025
Share :

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally akizungumzia maandalizi ya mchezo wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane utakaopigwa Benjamini Mkapa amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuvaa jezi nyekundu tu na siyo nyeupe wala rangi ya bluu ambazo ni miongoni mwa rangi zao za klabu.

SIMBADAY: SIMBA WALIVYOIGARAGAZA YANGA KWA MKAPA LEO....MBABE WA MANDONGA  AIBUA SHANGWE UWANJA MZIMA... | Soka La Bongo

“Kila Mwanasimba ambaye atakuja uwanjani Mei 25, 2025 jezi rasmi ni NYEKUNDU. Naomba, nasisitiza nyeupe ni rangi yetu, bluu ni rangi yetu lakini siku hiyo vaa jezi yekundu. Kama huna jezi nyekundu vaa hata t-shirt nyekundu. Mimi binafsi tavaa suti nyekundu, tai nyekundu na viatu vyekundu ili siku hiyo watu wote tuwe na rangi ya kufanana.”

“Lakini wewe mwenyewe Mwanasimba usiingie uwanjani kinyinge kama umeingia maabara. Ujue umekuja kwenye vita ya makelele, toa sauti hadi mwisho. Tuanze kujiandaa kuanzia sasa.”

“Kesho tutaondoka na watu wa aina tofauti tofauti tukiongozwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ambaye atatuongoza kwende ndege ya mama. Viongozi wa serikali, viongozi wa TFF na mashabiki watakuwepo.”- Semaji Ahmed Ally.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet