Mastaa punguzeni raundi za pombe msaidie yatima - Shishi
Eric Buyanza
October 17, 2025
Share :
Msanii na mfanyabiashara Zuwena Mohammed aka Shilole au Shishi Baby, amewataka mastaa wenzake kupunguza kuagiza raundi wanapokuwa kwenye starehe za unywaji pombe badala yake siku moja moja wajitoe kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima.
Akipiga stori na Mwanaspoti, Shilole aliwataka wasanii kuiga mfano wa watu ambao hujitoa kwa watoto yatima kwani kwa kufanya hivyo mambo yao mengi yatafunguka.
“Jamani mie nashauri kitu kimoja, tupunguze raundi za kuagiza pombe tunapokuwa kwenye starehe wasanii wenzangu, badala yake tujitoe sana kwa watoto yatima, ili mambo yetu yatuendee, ujue hata hawa watu wenye kipato kikubwa, siyo kwamba walilala na kuamka matajiri, wao wamekuwa wakijitoa sana kwenye jamii isiyojiweza,” amesema Shilole.
MWANASPOTI