pmbet

Mayele afikia level za Samatta Afrika

Sisti Herman

June 3, 2025
Share :

Baada ya juzi kuwa sehemu ya wachezaji muhimu wa klabu ya Pyramids walioiwezesha timu hiyo tajiri kutwaa Ubingwa wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, mshambuliaji Fiston Mayele ameweza kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo huku akiandika historia inayoenda kuwa sawa na ya mshambuliaji wa zamani wa Simba na TP Mazembe Mbwana Samatta.

Mayele raia wa Congo ameifikia rekodi ya Samatta raia wa Tanzania ya kuwa mfungaji bora kwenye michuano miwili ya CAF ya vilabu, yaani Ligi ya Mabingwa na Kombe la shirikisho.

Kama ilivyokuwa kwa Samatta kuwa mfungaji bora wa kombe la shirikisho Afrika akiwa na TP Mazembe mwaka 2013, Mayele alikuwa mfungaji bora wa kombe la shirikisho Afrka mwaka 2023 akiwa na Yanga.

Kama ilivyokuwa kwa Samatta kuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na TP Mazembe mwaka 2015, Mayele amekuwa mfungaji bora wa kombe la shirikisho Afrka mwaka 2025 akiwa na Pyramids.

Mchezaji mwingine aliyewahi kufanya hivyo kwenye Historia ya CAF ni Edward Sodomba raia wa Zimbabwe aliyekuwa mfungaji bora wa kombe la shirikisho Afrika mwaka 2011 na mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2012.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet