Mazishi ya Papa Francis kufanyika jumamosi April 26,2025.
Joyce Shedrack
April 22, 2025
Share :
Aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumamosi Aprili 26, 2025 kwenye Kanisa Kuu la Bikira Maria huko Roma Italia ambapo Kiongozi wa Chuo cha Makardinali, Giovanni Battista Re ataongoza mazishi hayo.
Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Vatcan imetoa taarifa hiyo muda mfupi uliopita ikisema tukio la mazishi litaanza majira ya saa tano asubuhi huko Vatcan.
Siku ya kesho mwili wa Papa Francis utawekwa kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican kwa ajili waumini kutoa heshima za mwisho.