Mbunge apigwa risasi akiwa kwenye gari Kenya
Sisti Herman
May 1, 2025
Share :
Mbunge wa Chama cha ODM, Charles Were amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye gari katika mzunguko wa Hifadhi ya City kwenye Barabara ya Ngong Jijini Nairobi kutoka kwa Watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki ambao bado hawajatambulika
Mbunge huyo wa Kasipul ambaye chama chake kinaongozwa na Raila Odinga amepigwa risasi Saa 1:30 Usiku, jana Aprili 30, 2025 ambapo mashuhuda wamesema mtu aliyempiga risasi alisogea karibu kabisa katika dirisha la gari na kufyatua risasi kisha kutokomea kusikojulikana
Alikimbizwa Hospitali lakini baadaye ikatangazwa amefariki, Jeshi la Polisi la Kenya bado halijatoa tamko kuhusu tukio hilo.