pmbet

Mbunge wa Viti Maalum, Halima Idd Nassor Afariki Dunia

Sisti Herman

January 18, 2026
Share :

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), ametangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Halima Idd Nassor, kilichotokea leo Jumapili, tarehe 18 Januari 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Spika, marehemu alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kufuatia tukio hilo, Mheshimiwa Zungu amesema Bunge na Taifa kwa ujumla limepoteza kiongozi muhimu aliyejitolea kulitumikia taifa kupitia nafasi yake ya uwakilishi.

“Natoa pole kwa Waheshimiwa Wabunge wote, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Spika.

Spika ameongeza kuwa Ofisi ya Bunge, kwa kushirikiana na familia ya marehemu, inaendelea kuratibu mipango ya mazishi, huku akibainisha kuwa taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kadri maandalizi yanavyoendelea.

Mheshimiwa Halima Idd Nassor alikuwa Mbunge wa Viti Maalum na alitambulika kwa mchango wake katika masuala ya kijamii na kisera ndani na nje ya Bunge.

“Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.” Amina.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet