Mechi ya JKT na Simba kupigwa Meja Isamuhyo.
Joyce Shedrack
May 2, 2025
Share :
Mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya mwenyeji JKT Tanzania dhidi ya Simba utapigwa kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo tofauti na taarifa za awali kuwa mechi hiyo itapigwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga.
Mtendaji Mkuu wa JKT Tanzania amekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni kuwa wameipeleka mechi hiyo nje ya Jiji la Dar es Salaam huku akisema mchezo huo kwenye uwanja wao wa nyumbani Mbweni.
"JKT TZ ni ya Dar es Salaam mechi yetu itapigwa Dar es Salaam kwenye uwanja wetu, marekebisho siyo lazima yaanze sehemu ya kuchezea.''Amesema Jemedar Said kupitia kipindi cha michezo cha Crown Fm.
Awali taarifa zilikuwa zinaeleza kuwa mechi hiyo imepelekwa mkwakwani kutokana na Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kufanyiwa ukarabati wa mwisho kuupa utayari wa kutumika kwa ajili ya mazoezi ya timu zitakazoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika wa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (CHAN) 2025 mwezi Agosti mwaka huu.
Mchezo huo utapigwa mapema mwezi wa tano siku ya tarehe 5 mwaka huu kwa mujibu wa ratiba ya Bodi ya Ligi.