Mfungwa aliyemshambulia rapa Tory Lanez visu 14 abainika.
Joyce Shedrack
May 14, 2025
Share :
Baada ya taarifa za Rapa Maarufu wa Canada kusambaa kuhusu kuchomwa kwake vizu 14 mnamo mei 12, upelelezi umebaini kuwa aliyehusika kwenye tukio hilo anafahamika kama Santino Casio ambae anatumikia kifungo cha maisha Gerezani kwa kesi ya mauaji ambayo aliyafanya huko nyuma tofauti na tukio hilo.
Taarifa za upelelezi huo zimesema kuwa ni kweli Tory Lanez alishambuliwa na mfungwa mwenzie ambae ni Casio akiwa gerezani majira ya saa 1:20 na kuchomwa visu 14, ambapo mfungwa aliyetenda kosa hilo kwa hivi sasa yupo katika chumba cha maojiano huko Gerezani.
Santino alifungwa Gerezani tangu 2004 akitumikia kifungo cha maisha kwa kufanya mauaji ya kutumia silaa, na bado akiwa Gerezani pia akawa na historia ya kujeruhi wafungwa wenzie kwa silaha kali, kwahiyo kwenye matukio haya ya kujeruhi si kwa mara ya kwanza kufanya hivyo.
Tory Lanez yeye kwa hivi sasa hali yake inazidi kutengamaa akiwa hospitali, licha ya kwamba akipona ataendelea na kutumikia jela mpaka ale atakapomaliza adhabu yake ya kifungo cha miaka yake 10 Gerezani.