pmbet

Millen Magese kuandaa rasmi Miss Universe Tanzania 2025

Sisti Herman

May 21, 2025
Share :

Millen Happiness Magese, mwanamitindo wa kimataifa na Miss Tanzania wa mwaka 2001, ameidhinishwa rasmi na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuandaa mashindano ya Miss Universe Tanzania 2025 kupitia kampuni yake, Millen Privé & Co, yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam.

 



Magese, ambaye pia ana leseni kutoka kwa Shirika la Miss Universe, amepongezwa na BASATA kwa kujitolea kwake kurejea Tanzania na kuchangia maendeleo ya tasnia ya urembo na mitindo nchini.

Katibu Mtendaji wa BASATA, Dk. Kedmon Mapana, amesema kuwa baraza litashirikiana naye ili kuhakikisha mashindano yanafanyika kwa uadilifu na kwa mujibu wa kanuni za maadili za kitaifa.

Magese ameonyesha shukrani zake kwa idhini hiyo na amesema ana mpango wa kuinua tasnia ya urembo na mitindo ya Tanzania.

Aidha, amemkaribisha Miss Universe Tanzania 2024, Judith Ngussa, kushiriki kikamilifu katika kumudu mashindano ya 2025, ikiwa ni pamoja na kuwashauri warembo wanaoshiriki.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet