Miloud Hamdi achaguliwa kuwa kocha bora wa Mwezi April.
Joyce Shedrack
May 3, 2025
Share :
Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi April kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara.
Hamdi amefanikiwa kubeba tuzo hiyo baada ya kuisadia klabu ya Yanga kuibuka na ushindi katika michezo yote minne waliyocheza mwezi huo na kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu.
Kocha huyo aliibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Tabora United,ikavuna alama tatu pia kwa Coastal Union kufuatia ushindi wa goli 1-0 huku ikiitandika Azam Fc mabao 2-1 na Fountain Gate magoli 4-0.