pmbet

Mimi nitakuwa mtu wa mwisho kutamani kuhama Chadema - Halima Mdee

Eric Buyanza

June 6, 2025
Share :

"Waliokwenda CHAUMMA, zao lao ni CHADEMA ni watu waliojenga CHADEMA kwa jasho na damu, waliobaki CHADEMA kuna watu ambao waliijenga lakini kuna watu wapya ambao wamekuja wamekuta matunda yapo tayari na wakafikiria wamefika kama vile hakuna watu waliojenga kwahiyo mimi zile zote mbili ni familia zangu"

 

"Tumetoka nao mbali lakini 'so far' mimi ni mwana CHADEMA bado kwahiyo kama kutakuwa bado na nafasi ya kufanya kazi mimi ni CHADEMA na kama CHADEMA itanifungia milango hainitaki basi nitaangalia mbadala mwingine"

 

"Lakini mimi nitakuwa mtu wa mwisho kutamani kuhama CHADEMA kwa sababu nimetumia nusu ya maisha yangu kuijenga CHADEMA lakini sasa milango ikifungwa na kuwekwa makameo siwezi kulazimisha"
- Halima Mdee

 

NIPASHE
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet