pmbet

Mji mzima walewa baada ya polisi kuchoma tani 20 za bangi

Eric Buyanza

May 13, 2025
Share :

Wakazi elfu 25 wa mji wa Lice, mkoani Diyarbakır nchini Uturuki, walijikuta wamelewa bila kupenda baada ya polisi kuchoma zaidi ya tani 20 za bangi iliyokamatwa katika mji huo.

Aprili 18, mamlaka nchini humo zilifanya operesheni ya kuchoma zaidi ya tani 20 za bangi, hali iliyosababisha hewa katika mji huo kuwa nzito kutokana na moshi mkubwa. 

Kwa takriban siku tano, watu hawakuweza kuacha madirisha yao wazi na kuepuka kutoka nje, kwa hofu ya kulewa na kupata dalili kama vile kizunguzungu, kichefuchefu na kushindwa kuona. 

Bangi iliyoharibiwa ilikuwa na thamani ya Lira za Uturuki Bilioni 10 (sawa na dola 261,433,808) ambazo ni takriban Milioni 700 za kitanzania.

Yahya Öğer, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Yeşil Yıldız, alisema ingawa mafanikio yanayopatikana na mamlaka katika vita dhidi ya dawa za kulevya ni muhimu, lakini njia iliyotumika kuharibu bangi hiyo haikuwa sahihi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet