pmbet

Mjue Valentina Vassilyeva, mwanamke aliyezaa watoto 69

Eric Buyanza

January 24, 2026
Share :

Idadi ya watoto ambao mwanamke anaweza kuzaa maishani mwake inategemea mambo mengi ya kibiolojia, afya, na mazingira.

Kulingana na Kitabu cha Rekodi za Dunia (Guinness World Records), mwanamke aliyewahi kuzaa watoto wengi zaidi alitwa Valentina Vassilyeva aliyeishi kwenye karne ya 18 (mwaka 1707–1782) huko Shuya nchini Urusi ambaye inasemekana alizaa watoto 69 na kufariki akiwa na miaka 76.
 

MCHANGANUO WA WATOTO WAKE
 

Kati ya mwaka 1725 na 1765, alijifungua mara 27 na kupata watoto 69 kama ifuatavyo:

Mapacha wawili (Twins): Seti 16 (watoto 32).
Mapacha watatu (Triplets): Seti 7 (watoto 21).
Mapacha wanne (Quadruplets): Seti 4 (watoto 16).

Ingawa rekodi ya Valentina ni ya kihistoria, kuna wanawake wengine katika nyakati za hivi karibuni wanaojulikana kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto:

Mariam Nabatanzi (Uganda): Anajulikana kama "Mama Uganda," amejifungua jumla ya watoto 44 kufikia mwaka 2019 (38 kati yao wako hai).

Halima Cissé (Mali): Anashikilia rekodi ya dunia ya sasa ya kujifungua watoto wengi zaidi kwa mkupuo mmoja (watoto 9) waliozaliwa Mei 2021.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet