pmbet

Mkuu wa Mkoa ateketeza ekari 3 za bangi Tabora

Sisti Herman

June 8, 2025
Share :

Kamati ya ulinzi na usalama Mkoani Tabora imeteketeza zaidi ya ekari Tatu za shamba la bangi lililolimwa na Watu wasiojulikana,katika hifadhi ya misitu mbuga ya nyahua wilayani sikonge mkoani hapo huku Jeshi la Polisi likitangaza operesheni maalumu ya kuwasaka Watu hao.

 



zoezi hilo la kuteketeza Shamba la bangi hiyo limeongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ambapo mara baada ya kutamatika kwa zoezi hilo akatoa kauli ya Serikali na kusema kuwa kamati hiyo haitavumilia vitendo vya uhalifu wa aina hiyo vinavyohatarisha afya za Wananchi na kuahidi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika hifadhi zote za Mkoa huo.

Kwa upande wake kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tabora kamishina mwandamizi wa Jeshi la Polisi,Richard Abwao ametangaza operesheni maalumu ya kuwasaka watu hao waliojihusisha na kilimo hicho haramu pamoja na wasambazaji na watumiaji wa zao hilo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet