Mnyama kuwafuata RS Berkane kesho.
Joyce Shedrack
May 12, 2025
Share :
Klabu ya Simba inatarajia kuondoka Nchini siku ya kesho Mei 13, 2025 saa 11:00 Alfajiri kuelekea Nchini Morocco kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane utakaopigwa Mei 17, 2025.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amethibitisha hilo kwenye Mkutano na waandishi wa Habari na kuweka wazi kuwa safari hiyo itakuwa ya masaa saba 7 kutoka Dar es Salaam hadi Casablanca huku akimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha safari hiyo.
“Kikosi kitaondoka kesho saa 11 alfajiri kwenda Morocco itakuwa safari ya masaa 7 saba moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Casablanca".
“Kwa hili hatuna budi kumshukuru sana, tena kumshukuru tena, tena kumshukuru mara elfu, kumshukuru pakubwa Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wetu wa Tanzania. Kwa hili ametutendea kubwa sana”.Amesema Ahmed Ally.