Mohammed Al-Ghamari, kiongozi wa waasi wa Houthi afariki dunia
Eric Buyanza
October 17, 2025
Share :
Waasi wa Houthi wa nchini Yemen wametangaza kifo cha kiongozi wao wa kijeshi, Jenerali Mohammed al-Ghamari.
Waasi wa Houthi hawakueleza mazingira ya kifo chake, lakini Waziri wa Ulinzi wa Israel amesema kuwa Mohammed al-Ghamari alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata katika shambulio la Israel la mwezi Agosti.
Katika shambulio hilo aliuawa pia liliua Waziri Mkuu wa Houthi na maafisa wengine kumi na wawili. Tangu kuanza kwa operesheni ya Israel huko Gaza, waasi wa Houthi wamedai kuwaunga mkono Wapalestina na wamekuwa wakifanya mashambulizi katika ardhi ya Israel.
Mohammed al-Ghamari alikuwa mmoja wa washirika wa karibu wa kiongozi wa Houthi Abdul-Malik al-Houthi na mmoja wa wanajeshi wenye uzoefu mkubwa. Alikuwa mkuu wa shirika la operesheni za hivi karibuni dhidi ya Israel.
Taarifa ya Houthi iliyotolewa jana haikutaja moja kwa moja kuhusika kwa Israel.