Morocco kujenga uwanja mkubwa zaidi wa mpira duniani.
Joyce Shedrack
November 21, 2024
Share :
Taifa la Morocco limepanga kuanza ujenzi wa uwanja walioupa jina la Grand Stade Hassan II karibu na Jiji la Casablanca ukiwa na uwezo wa kubeba watu 115,000 ambao utakuwa ndio uwanja mkubwa zaidi wa mpira wa miguu barani Afrika na Duniani kwa ujumla.
Morocco wanatarajia kukamilisha ujenzi wa uwanja huo kabla ya mwaka 2030 ili utumike kwenye fainali za mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2030 zilizopangwa kufanyika kwenye Nchi tatu ikiwa ni Hispania,Ureno na Morocco.
Nchi hizo mbili kutoka Barani Ulaya zimepanga kushirikiana na Morocco katika ujenzi huo ikiwa ni maandalizi makubwa kuelekea Nchi hizo kuwa wenyeji wa mashindano hayo makubwa zaidi duniani.