Moshi mweupe wategemewa Vatican leo
Sisti Herman
May 8, 2025
Share :
Baada ya moshi mweusi kuonekana mwisho wa siku ya kwanza ya mkutano wa uchaguzi wa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Mei 07 ukiashiria kutopakana kwa Papa, matarajiio ya waumini wa kanisa hilo ni moshi mweupe Vaytica leo.
Makadinali 133 wanashiriki uchaguzi wa Papa wa 267 baada ya kifo cha Papa Fransisko Jumatatu ya Pasaka Aprili 21.
Maelfu waliokusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mt Petro, Vatican City walishuhudia moshi huo mweusi ukitoka kwenye bomba la moshi lililopo kanisa dogo la Sistine na baadaye wakatawanyika.