Mr. Beast Bilionea mdogo zaifi ambaye hajarithi utajiri
Sisti Herman
May 23, 2025
Share :
Mtengeneza maudhui mtandaoni Jimmy Donaldson au MrBeast amekuwa bilionea wa kwanza mwenye umri chini ya miaka 30 kwa pesa ambazo sio za urithi.
Akiwa na umri wa miaka 27, MrBeast amefikia utajiri wa dola bilioni 1 kupitia juhudi zake binafsi, bila kurithi mali yoyote. Hii inamtofautisha na mabilionea wenzake walio chini ya miaka 30 ambao wengi wao walirithi utajiri kutoka kwa familia zao.
MrBeast alianza safari yake ya YouTube akiwa na miaka 12, na alipata umaarufu mkubwa mwaka 2017 baada ya kuhesabu namba moja hadi 100,000 kwa mfululizo.