pmbet

Mtoto wa Ronaldo aanza kukipiga timu ya Taifa ya Ureno

Sisti Herman

May 12, 2025
Share :

Mtoto wa Cristiano Ronaldo, Cristiano Ronaldo Jr., ambaye ana umri wa miaka 14, ameanza mazoezi na timu ya taifa ya Ureno ya vijana chini ya umri wa miaka 15 (Under-15).
 


Hii ni mara yake ya kwanza kuitwa katika timu hiyo, na atashiriki katika mashindano ya kimataifa ya vijana yanayoitwa Vlatko Marković International Tournament huko Kroatia kuanzia Mei 13 hadi 18, 2025.

Ureno itacheza dhidi ya Japan, Ugiriki, na England pamoja na mpinzani mwingine ambaye bado hajatangazwa.

Ronaldo Sr. alionyesha furaha yake kwa kuweka picha ya orodha ya wachezaji kwenye Instagram yake na ujumbe "Proud of you, son!"

Ronaldo Jr. amekuwa akicheza katika akademi ya vijana ya Al-Nassr huko Saudi Arabia, ambapo baba yake anachezea klabu hiyo, na hapo awali amewahi kuwa katika akademi za Juventus, Manchester United, na Real Madrid.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet