Mtuhumiwa mauaji ya Tupac Shakur anyimwa dhamana.
Joyce Shedrack
August 31, 2024
Share :
Jaji wa Mahakama ya Wilaya ya Clark Nchini Marekani Carli Kierny amemnyima tena dhamana mtuhumiwa wa maujai ya mwanamuziki Tupac Shakur, Duane “Keffe D” Davis mauaji yaliyotokea mwaka 1996 Jijini Los Angeles.
Keffe D ambaye mara kwa mara amekuwa akiomba dhamana ameomba dhamana kwa mara nyingine ili aweze kwenda kupatiwa matibabu lakini mahakama hiyo imemkatalia dhamana toka alivyokamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2023.
Kierny ambaye ni jaji wa mahakama hiyo ameweka wazi sababu ya kutokupokea dhamana hiyo ni kutokana na kuwa na hisia mbaya zinazojaribu kufichwa na mtoaji wa dhamana hiyo ambaye ni "Wack 100".
Keffe D amekana mashtaka ya mauaji ya daraja la kwanza na kesi hiyo imesogezwa mbele kutoka Novemba 4, 2024 hadi Machi 17 mwakani itakaporindima tena.