"Muda Mzuri wa Mazishi ni saa 10 jioni" Ahmed Ally.
Joyce Shedrack
April 15, 2025
Share :
“Muda mzuri wa mazishi huwa ni saa 10 jioni, muda mzuri wa kumzika mtu huwa ni saa 10 na sisi muda wetu tukitaka kufanya Ubaya Ubwela na huwa tunafanikiwa kabisa huwa ni saa 10 jioni. Tukutane Uwanja wa Amaan, mechi ni sa 10:00 jioni. Wanaotoka Dar es Salaam wajue kabisa muda wa mchezo wasijesema wamekariri muda wa saa 2:15 usiku.”
“Kama kawaida yetu, sisi ni watu wa hekaheka. Pamoja na kuwa na uwezo wa kumaliza tiketi ndani ya muda mfupi lakini asili yetu ni hamasa, kupita na kispika, mtaa kwa mtaa na hata tiketi zikiisha leo, hamasa yetu ipo pale pale. Tunatarajia kuanza hamasa siku ya Alhamisi Aprili 17, 2025 na tutaanzia Tawi la Mkwajuni lililopo mkoa wa Kaskazini Unguja.”
“Ijumaa tutatoa msaada kwenye kituo cha kutunza watoto yatima na kwenye hili tutashirikiana na Taasisi ya Mo Dewji lakini pia tunawakaribisha Wanasimba wote kuungana kutoa misaada. Hiyo itakuwa Siku ya Kitaifa ya Simba kutoa misaada kwenye vituo vya watoto yatima, hospitali kwa wahitaji ili kuwa karibu na Mungu atusaidie tarehe 20. Ukiweka nia kwamba Mungu natoa sadaka hii ili Simba yangu ishinde, Mungu ataipokea."- Semaji Ahmed Ally akiongea na wanahabari visiwani Zanzibar.