Muigizaji mkongwe wa India Dharmendra Kewal Khrishan afariki dunia.
Joyce Shedrack
November 24, 2025
Share :
Muigizaji mkongwe wa filamu kutoka Nchini India Dharmendra Kewal Krishan almaarufu ‘Simple Man’ amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89 siku ya leo Novemba 24, 2025 Jijini Mumbai Nchini India.
Dharmendra ambaye mmoja wa waigizaji maarufu zaidi katika historia ya sinema ya India ametamba katika filamu zaidi ya 300 zikiwemo 'Sholay, Satyakam, Chupke Chupke, Yaadon Ki Baaraat, Loafer, Blackmail, Jugnu na nyingine nyingi.
Staa huyo aliyekuwa na wake wawili ameacha watoto sita ambao Sunny Deol, Bobby Deol, Vijeta Deol na Ajeeta Deol kutoka kwa mke wake wa kwanza, Prakash Kaur, watoto wengine wawili Esha Deol na Ahana Deol kutoka kwa mke wake wa pili Hema Malini.





