Mungu akubariki, asema Kaka akimkaribisha Ancelotti Brazil
Eric Buyanza
May 13, 2025
Share :
Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Kaka amemkaribisha Carlo Ancelotti kufuatia uteuzi wake wa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil.
Kaka, ambaye alicheza chini ya Ancelotti wakati akifundisha AC Milan, kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:
"Karibu, Bwana Ancelotti! Mungu akubariki!"
Ancelotti ndiye meneja aliyefanikiwa zaidi katika historia ya Real Madrid. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 65 alishinda mataji 15 katika misimu yake miwili akiwa na wababe hao wa LaLiga ya Uhispania.