pmbet

Museveni asaini sheria, raia kushtakiwa mahakama ya kijeshi

Eric Buyanza

June 16, 2025
Share :

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesaini sheria yenye utata inayoruhusu mahakama ya kijeshi kuwahukumu raia, chini ya hali zitakazochukuliwa kuwa za kipekee. 

Wakosoaji wanasema sheria hiyo mpya inakiuka uamuzi wa Mahakama ya Juu Zaidi mapema mwaka huu ambao uliwazuia raia kuhukumiwa na jeshi.

Kulingana na sheria hiyo raia yeyote atakayepatikana na silaha kinyume cha sheria atawasilishwa katika mahakama ya kijeshi. 

Taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa X wa bunge la nchi hiyo inasema 
"Rais Kaguta Museveni ameidhinisha Sheria ya Vikosi vya Ulinzi ya 2025. iliyofanyiwa marekebisho."

Bunge la nchi hiyo mwezi uliopita lilipitisha Muswada wa Marekebisho ya Jeshi la polisi nchini Uganda UPDF, ukitaka kuidhinisha jeshi kuhukumu raia. 

Wabunge wa upinzaji walipinga kikao hicho katika maandamano, wakisema kuwa hatua hiyo ilikiuka uamuzi wa Mahakama ya Juu Zaidi wa mwezi Januari ambayo ilipiga marufuku kesi za raia kusikilizwa katika mahakama ya kijeshi. 

Wakati wa kupitishwa kwa muswada huo kulikuwa na wanajeshi wengi ndani na nje ya Bunge.

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet