pmbet

Mwaka 2025 watu watanitafuta kwa tochi – Irene Uwoya

Eric Buyanza

December 28, 2024
Share :

Nyota wa filamu nchini, Irene Uwoya amekiri hakuna kitu kilichobaki kuwa kumbukumbu kwake kwa mwaka 2024 isipokuwa uamuzi wake wa kuamua kuokoka.

"Kuna mambo mengi sana maovu nimeyafanya na yamefanywa kuhusu mimi katika mwaka 2024, sasa sitaki mwaka 2025 kubeba matatizo ya mwaka huu na kuingia nayo mwaka mpya, nitakuwa mpya na wa tofauti sana na watu watanitafuta kwa tochi, ila kikubwa ninachoshukuru na kitu ambacho kimenifurahisha kwa mwaka huu 2024 ni kuweka wazi kuokoka kwangu," anasema Irene.

"Kitu ambacho naona nimefanya kikubwa sana kwa mwaka huu 2024 ni hilo, japo najua watu wananisema sana, lakini maadam nishatoa kitu kilichokuwa kinanisumbua ambacho kilitakiwa watu wote wajue ili niwe na amani ya moyo wangu ni haya mabadiliko yangu, wala sijali nazidi kusonga mbele tu kwa sasa." 

👉MWANASPOTI

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet