Naibu IGP ajiuzulu kisa kifo cha Mahabusu
Sisti Herman
June 16, 2025
Share :
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Kenya Eliud Lagat ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake kwenye jeshi hilo.
Katika taarifa, Lagat ameeleza kuwa amechukua uamuzi huo ili kuruhusu mamlaka kufanya uchunguzi wa kifo cha mwanablogu Albert Ojwang, baada ya yeye kutajwa kama mtu anayetakiwa kutoa maelezo zaidi katika uchunguzi unaoendelea wa mauaji hayo.