Namibia ilivyomuapisha Rais wake wa kwanza mwanamke
Eric Buyanza
March 22, 2025
Share :
Namibia Ijumaa ya jana ilimuapisha rais wake wa kwanza mwanamke Netumbo Nandi-Ndaitwah, aliyeshinda uchaguzi mwaka jana na kurefusha muda wa miaka 35 wa chama tawala cha SWAPO mamlakani.
Nandi-Ndaitwah mwenye umri wa miaka 72 amekuwa mmoja wa viongozi wachache wa kike barani Afrika, katika sherehe iliyohudhuriwa na marais kutoka nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Angola, Afrika Kusini na Tanzania.
Vifijo na nderemo zilisikika mara baada ya Netumbo kula kiapo.
Rais aliyemaliza muda wake Nangolo Mbumba mwenye umri wa miaka 83, amekabidhi madaraka kwa Ndaitwah katika hafla iliyofanyika katika siku ya kusherehekea kumbukumbu ya uhuru wa nchi hiyo.
Hafla hiyo ilihamishwa kutoka uwanja wa uhuru nchini humo na kufanyika katika ikulu kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.