Nandy na Billnass wanogesha penzi...! Mtoto wa pili yuko njiani.
Joyce Shedrack
August 15, 2024
Share :
Wasanii wa muziki wa bongofleva Billnass pamoja na Nandy huwenda wakawa wanatarajia kupata mtoto wa pili kutokana na comment aliyondosha mrembo huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya kupostiwa na mume wake.
Siku ya leo msanii Billnass amechapisha video ya mke wake kwenye ukurasa wake wa instagram aliyoambatanisha na ujumbe wa "MUNGU ANIPE NINI TENA ❤️. HUYU NDO NAMBA MOJA SASA" kisha Nandy aka-comment BABA KIJA....😻". ujumbe ulioacha maswali mengi kwa mashabiki kwamba je Nandy ni mjamzito?.
Wawili hao ambao hivi karibuni wametimiza miaka miwili ya ndoa yao tayari wana mtoto mmoja wa kike anayejulikana kama Naya Bill .