Nandy na Billnass washerekea miaka 3 ya ndoa yao.
Joyce Shedrack
July 16, 2025
Share :
Msanii wa muziki wa Bongofleva Billnas na mke wake ambaye pia ni staa wa muziki Nandy siku ya leo wametimiza miaka mitatu ya ndoa tangu walipofunga ndoa yao Julai 16 mwaka 2022 katika Kanisa la KKKT Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Wawili hao wanasherekea miaka mitatu ya ndoa yao wakiwa wamejaliwa Binti mmoja Naya aliyezaliwa miezi michache tu baada ya wasanii hao kufunga ndoa.
Mbali na muziki, katika ndoa yao kila mmoja ana biashara zake moja au mbili anazojishughulisha nazo, @officialnandy ana lebo yake, The African Princess, anauza bidhaa za urembo na ana kampuni inayohudumia maharusi, huku @billnass akiuza bidhaa za kieletroniki hasa simu.