pmbet

Natamani mama angekuwa hai afurahie mafanikio yangu - Johari

Eric Buyanza

August 6, 2025
Share :

Msanii wa Bongo Movie, Johari amesema kukosekana kwa mama yake kunamuumiza sana kwani angekuwepo angefurahia mafanikio yake.

Akizungumza katika siku yake ya kumbukizi ya kuzaliwa hivi karibuni, Johari alisema mara kwa mara huwa anahisi pengo kubwa katika maisha yake ambalo liliachwa na mama yake miaka saba iliyopita. 

Alisema anatamani mama yake angekuwa karibu naye leo hii kufurahia sehemu ya kile ambacho Mungu amembariki nacho. 

Kwa mujibu wa Johari angetamani sana mama yake kuchuma matunda ya mafanikio yake, kwani alimshuhudia akiwahangaikia wakati akiwa mdogo. 

Source: Mwanaspoti

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet