pmbet

"Neymar ni mchezaji wa kwanza kuitwa kufanya kazi akiwa nyumbani"Rais wa Brazil.

Joyce Shedrack

June 20, 2026
Share :

Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva ametoa kauli iliyozua gumzo kuhusu nyota wa soka kwenye Taifa hilo Neymar Jr baada ya kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, akitania kwamba mshambuliaji huyo aliyejeruhiwa ndiye mchezaji wa kwanza anayefanya kazi akiwa mbali kuitwa kwenye Kombe la Dunia.

Brazil president Lula pokes fun at Neymar over World Cup injury absence -  Yahoo Sports

Wakati wa kipindi cha matangazo nchini Brazil, Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva alimuuliza kijana mdogo ni nani mchezaji bora zaidi wa Brazil? akajibiwa kuwa ni Neymar.

 

Rais Lula akasema “Kijana, Neymar ndiye mchezaji wa kwanza kabisa kuitwa kwenye Kombe la Dunia huku akifanya kazi kutoka nyumbani (home office)!”

 

Neymar ndiye mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Brazil, akiwa amefunga mabao 79 katika mechi za kimataifa, rekodi iliyomwezesha kumpita Pelé katika vitabu vya historia.

 

Kombe hili la Dunia ni la nne kwake kushiriki, baada ya kucheza katika mashindano ya mwaka 2014, 2018 na 2022, ambapo alifunga jumla ya mabao manane katika matoleo hayo matatu.

 

Kocha Mkuu wa Brazil Carlo Ancelotti amethitibisha kuwa nyota huyo atakuwa tayari kucheza katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Scotland.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet