Nilikosea sana kutoka na wanaume masikini - Tiwa Savage
Eric Buyanza
August 9, 2025
Share :
Mwanamuziki wa Nigeria, Tiwa Savage, amesema alifanya makosa katika mahusiano yake ya awali kwa kuingia kwenye mahusiano na wanaume ambao hawana uwezo mkubwa wa kifedha kuliko yeye.
Hitmaker huyo wa ‘Koroba’ anasema kwa sasa amejirekebisha na kama ataingia kwenye mahusiano basi itakuwa na wanaume wenye pesa (matajiri).
"Nimejaribu njia nyingine kwa miaka mingi. Acha sasa nijaribu nione inakuaje kuwa na mwanaume mwenye pesa." alisema Tiwa
Itakumbukwa Tiwa Savage alifunga ndoa na meneja wake wa zamani Tunji Balogun, almaarufu Teebillz, mwaka wa 2013 lakini walitalikiana mwaka 2018 baada ya majaribio ya kusuluhisha tofauti zao kushindikana.
Ndoa yao ilizaa mtoto wa kiume anayeitwa Jamil.