Nililia nilipozaa mtoto wa kiume, nilitaka wa kike – Tiwa Savage
Eric Buyanza
January 19, 2026
Share :

Mwanamuziki wa Nigeria Tiwa Savage amefichua kuwa hakufurahishwa kabisa alipojifungua mtoto wa kiume na kudai kuwa alitoa machozi baada ya kupewa taarifa ya jinsia ya mtoto wake.
Akiongea kwenye mahojiano ya hivi karibuni na Korty EO, Savage alisema siku zote alikuwa akitamani mtoto wa kike, na kitendo cha kujifungua wa kiume kulimfanya akose ukaribu wa dhati na mtoto huyo kwa miaka miwili ya mwanzo.
Savage anakumbuka baada ya kutoka kujifungua kampuni ya Pepsi nchini Nigeria walimnyima dili kutokana na muoekano wake kubadilika, jambo lililosababisha aone mtoto huyo wa kiume amekuja kumharibia kazi yake.
“Kusema ukweli sikuwahi kuwa na uhusiano wa karibu na mwanangu kwa miaka miwili ya mwanzo. Siku zote nilitaka mtoto wa kike...waliponiambia ni wa kiume nililia sana.”
"Alipozaliwa alikuwa akilia kila mara na mwili wangu haukurudi kama ulivyokuwa awali, nilionekana mbaya"
"Nilikuwa nina kampeni ya kufanya na Pepsi wakati huo na walinikataa. Nikawa na mawazo kichwani kuwa huyu mtoto wa kiume amekuja kuniangamiza. Lakini sasa hivi ni rafiki yangu mkubwa, "Savage alisema.





