Nilinusurika kupigwa wakidhani ni mchawi – Bi Mwenda
Eric Buyanza
May 3, 2025
Share :
Muigizaji mkongwe Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ amesema ameacha kuigiza nafasi za ‘kichawi’ baada mashabiki zake kumhisi ni mchawi kweli.
Bi Mwenda alisema kuna siku alitaka kupigwa na watu maeneo ya Tandika Sokoni, kisa tu kufikisha kwake ujumbe kupitia sanaa wakidhani kweli ni mchawi.
“Najua kazi nimeifanya ya kufikisha ujumbe kwenye vipengele vya kucheza mwanamke mchawi, lakini nimeona niachane navyo kwa sasa, kwa umri wangu unavyozidi kwenda mashabiki zangu wananihisi kweli mimi ni mchawi. Nilishawahi kutaka kupigwa sokoni Tandika kwa kudhaniwa ni mchawi nafanya chuma ulete kwenye biashara za watu, aisee sitaki tena hiyo nafasi,” alisema Bi Mwenda.
MWANASPOTI