Nyakati ngumu pia zina nafasi katika maisha yetu - Yao Kouassi
Eric Buyanza
May 20, 2025
Share :
Beki wa kulia wa Yanga, Yao Kouassi amesema maisha ya mchezaji wa mpira si ya mafanikio tu, pia kuna nyakati ngumu hukutana nazo.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Yao ameweka picha aliyofanyiwa upasuaji wa goti na kuweka ujumbe kuonesha ni namna gani anapitia maumivu kwa sasa.
Katika ujumbe huo amesema: “Tuwe na utamaduni wa kukubali kwamba si kila kitu katika maisha yetu kinapaswa kuwa chepesi au kizuri kila wakati.
“Kushinda kweli kunakuwepo na nyakati ngumu pia zina nafasi katika maisha yetu. Kila mtu anaweza kupitia changamoto yote ni suala la muda na kufanya kazi kimya kimya ili kurudi kileleni,"amesema beki huyo ambaye ana muda mrefu yupo nje ya uwanja kutokana na majeraha.