Nyoka asitisha huduma za treni nchini Japan
Eric Buyanza
May 2, 2025
Share :
Huko nchini Japan huduma za usafiri wa treni za mwendokasi za Shinkansen kutoka mji wa Tokyo kuelekea Osaka zilisimama kwa muda baada ya nyoka kujifungafunga kwenye nyaya za umeme.
Nyoka huyo mwenye urefu sentimita 40 alisababisha hitilafu ya umeme baada ya kufa alipokuwa akijaribu kutambaa kwenye waya zenye umeme mwingi na kusababisha huduma kusimama kwa dakika 17.
Shinkansen ni mtandao wa reli ya mwendokasi ambayo Japan ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuzindua huduma ya aina hiyo.