Old Trafford kumpokea Matheus Cunha mwishoni mwa msimu
Eric Buyanza
May 20, 2025
Share :
Matheus Cunha anatarajiwa kujiunga na Manchester United baada ya msimu kumalizika wikiendi hii, imeripoti Sky Sports.
Licha ya vilabu vingine kumtaka lakini mbrazil huyo anayekipiga na Wolves anataka kuichezea United na taarifa zinasema dili la uhamisho huo linakaribia kuiva.
Pamoja na kwamba klabu hiyo inapitia kipindi kigumu kwenye kupata matokeo, mbrazil huyo anaona sio kikwazo cha kumfanya asihamie Old Trafford.
Kwa sasa Man U wako nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi.
Chanzo kimoja kiliiambia Sky Sports, kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 "anaipenda United".
Cunha alisajiliwa na Wolves kutoka Atletico Madrid mwaka 2022.