pmbet

Oscar Oscar atangaza ujio wa ngoma mpya itakayosikilizwa na watoto.

Joyce Shedrack

May 23, 2025
Share :

Mtangazaji aliyejiingiza kwenye sanaa ya muziki wa Hip Hop Oscar Oscar leo ameahidi kuwa wimbo wake ujao utafuata maadili na utasikilizwa na watu wote wakiwemo watoto mara baada ya kumaliza kusoma kitabu cha maadili kutoka bodi ya filamu.

Ikumbukwe, siku ya jana Oscar aliitikia wito katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) ambapo aliitwaa baada ya kuachia wimbo wake wa kwanza 'Niombeeni' huku akipewa mwongozo maeneo ambayo utasisikia.

Basata imetoa mwongozo kwamba wimbo huo utapigwa kwenye kumbi za starehe, katika vyombo vya habari utapigwa kuanzia saa sita usiku. Pia hautapigwa kwenye vyombo vya usifiri wa umma na kwenye matamasha kama kuna watoto.
 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Oscar Oscar ametangaza ujio wa ngoma mpya ambao utazingatia maadili.

“Nimemaliza kusoma muongozo wa Adili ya Sanaa niliyopewa jana BASATA na nimeelewa vema. Leo naelekeza Zanzibar kuandika Wimbo wangu Mpya. Nitajitahidi Ngoma inayofata iwe inaweza kusikilizwa hata na Mtoto aliyezaliwa leo. MNIOMBEE 🙏🏻” Ameandika Oscar Oscar.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet